Saturday, May 19, 2012

JACKIE CHAN ASTAAFU FILAMU ZA MAPIGANO...

Siku za mapambano mbele ya kamera sasa zimekwisha!
Hiyo ni kauli aliyoitoa mkali wa filamu za mapambano na mapigano, Jackie Chan ambaye ametangaza rasmi kuacha kucheza filamu zake za aina hiyo zilizompa umaarufu kwa zaidi ya miaka 10 sasa.
Mkali huyo ambaye sasa ana miaka 58 alisema hayo wakati wa kuinadi filamu yake mpya ambayo ni ya 100 iitwayo 'Chinese Zodiac' jana alipoongea na waandishi wa habari akisema, "Hii itakuwa filamu yangu ya mwisho ya mapigano."
Alifafanua, "Nawaambia, mimi sasa nimekuwa mzee, hakika nimechoka mno."
Chan aliongeza, "Dunia ya sasa imejaa ghasia. Ni njiapanda kwa sababu napenda mapigano, lakini sipendi ghasia."

Aliendelea, "Sitaki kuwa nyota wa mapigano... Nataka kuwa mwigizaji wa ukweli. Nataka kuwa Robert De Niro wa Asia."
Chan amepata majeraha yasiyohesabika wakati wa kuandaa sinema zake, na kumbukumbu zinasema alionekana kwa mara ya kwanza kama mfungwa gaidi kwenye moja ya filamu bora za Bruce Lee ya "Enter the Dragon" mwaka 1973.

No comments: