Kwa wale waliofuatilia mechi ya kufunga pazi la Ligi Kuu England mwishoni mwa wiki iliyopita kati ya Manchester City na Queen's Park Rangers watakumbuka tukio la Nahodha wa QPR, Joey Barton kumpiga mshambuliaji wa Man City, Carlos Tevez (kama anavyoonekana pichani, wa tatu kutoka kulia) na kisha nahodha huyo kupewa kadi nyekundu. Kitendo hicho kiliigharimu timu yake na kwa upande mmoja kikainufaisha Man City iliyoibuka na ushindi wa mabao 3-2 na hivyo kuweza kutwaa ubingwa kwa mara ya kwanza baada ya miaka 44. Lakini Joey ambaye jina lake halisi ni Joseph Barton sio jina geni katika wachezaji watukutu. Vifuatayo ni baadhi tu ya vitimbi vyake:-
Mei 2005: Alitimua mbio an kwenda kumvunja mguu mtembea kwa miguu mwenye miaka 35 usiku wa manane mjini Liverpool.
Juni 2005: Alipigana na shabiki wa Everton mwenye miaka 15 kwenye hoteli iliyofikia timu ya Manchester City mjini Bangkok na akatozwa faini na klabu yake.
Septemba 2006: Alivua bukta yake mbele ya mashabiki wa Everton kwenye Uwanja wa Goodison Park. Alitozwa faini na kupewa onyo na Chama cha Soka England (FA).
Machi 2007: Alikamatwa kwa tuhuma za kumdunda dereva teksi aliyekataa kumsubiri kwenye mgahawa wa McDonald mjini Liverpool. Baadaye alifutiwa mashitaka baada ya binamu yake, Joshua Wilson kukiri kumpiga dereva huyo.
Mei 2007: Alimtukana Ousmane Dabo kwenye Uwanja wa Mazoezi wa Machester City.
Desemba 2007: Alinaswa na kamera za CCTV akimtandika ngumi mara kadhaa mtuhumiwa wake usoni kwenye mgahawa wa McDonald mjini Liverpool.
Mei 2008: Alifungwa jela miezi sita kwa udhalilishaji.
Mei 2009: Alisimamishwa kwa kumuapiza Shearer kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Novemba 2010: Alikiri makosa ya kumpiga ngumi mchezaji Blackburn Rovers, Morten Gamst Pederson na akafungiwa mechi tatu.

No comments:
Post a Comment