Pichani (juu): Ombaomba hao wakicheza kamari kando ya barabara mbele ya mtaa wenye mahoteli na migahawa maarufu. Chini: wakijisaidia kwenye moja ya uzio wa hoteli maarufu jijini London.
Zaidi ya ombaomba 50 kutoka nchini Romania waliotimuliwa kutoka eneo la Marble Arch jijini London wamesogea hatua chache kutoka eneo lenye hadhi kubwa jijini humo ya Park Lane.Kundi hilo limeweka kambi kwenye hifadhi ya barabara wakitazamana na mtaa uliosheheni misururu ya mahoteli na migahawa mikubwa jijini humo.
Wamekuwa wakirandaranda mitaani kuzunguka mitaa ya Marble Arch na Oxford mwezi uliopita wakati wafanyakazi wa Halmashauri ya Jiji wakipambana vitisho kutoka kwa Waromania kuelekea Michezo ya Olimpiki.

No comments:
Post a Comment