Monday, May 7, 2012

MAISHA YA WHITNEY WIKI MOJA KABLA YA KIFO CHAKE YAANIKWA...


KUSHOTO: Whitney akiwa na Ray J. KULIA: Akiwa na mbunifu wake wa nywele siku moja kabla ya kifo chake.
Kifo chake cha ghafla akiwa na umri wa miaka 48 kwenye Hoteli ya Beverly Hills kimeibua hisia na uvumi kuhusu tuhuma za utumiaji wa dawa za kulevya na mahusiano binafsi yenye utata.
Na sasa, jarida moja limeibua mapya kuhusu maisha binafsi ya Whitney Houston na siku zake za mwisho jijini Los Angeles, miezi mitatu baada ya kukutwa amekufa ndani ya bafu la hoteli.
Moja ya dondoo kwenye habari iliyoandikwa humo imemnukuu mchumba wa zamani wa aliyekuwa mume wa Whitney, Bobby Brown ambapo akikumbushia mzozo kati yake na mpenzi wa mwimbaji huyo, Ray J mwaka 2006.
Katika makala hiyo ndani ya jarida la Vanity Fair yenye kichwa kinachosomeka 'The Devils in the Diva', Karrine Steffans anakumbuka simu aliyopigiwa na Ray mara baada ya Whitney kuachana na Brown.
"Alisema, "Bado unaishi pamoja na Bob (Bobby Brown)?" anakumbuka Steffans. "Nikajibu, "Ndiyo, anaishi hapa."
"Kisha Ray akasema, "Mwambie nitatembea na wasichana zake wote, wewe na sasa mke wake."
Akijibu kauli ya Bobby katika mahojiano na kipindi cha televisheni cha 'The Today Show' wiki iliyopita ambapo alikana kumuingiza Whitney kwenye dawa za kulevya, Steffans alisema, "Jambo kubwa kwa Bob ni kwamba kila mtu anamlaumu kutokana na kuporomoka kwa Whitney, lakini alipokutana naye alikuwa tayari akitumia dawa za kulevya.
"Mara zote alikuwa akichukizwa na hilo. Alinieleza, "Yule wote wanayemuona sio Whitney halisi".
Alikuwa akisema mara kwa mara wakiwa faragha kwamba aliyekuwa akionekana katika kipindi cha 'Being Bobby Brown' ndiye Whitney halisi.
Kipindi cha 'Being Bobby Brown' kimekuwa kikirushwa nchini Marekani mwaka 2005 na kutengenezwa mfululizo wa vipindi maalumu Whitney alipoolewa na mwimbaji huyo ambavyo vilikoma baada ya kuachana mwaka 2007.
Ray J alikuwa akionekana na Whitney kwa nyakati tofauti wiki moja kabla ya kifo chake, huku picha yao ya mwisho ikipigwa siku mbili kabla ya kifo chake.
Picha zote za Whitney anaonekana akiwa amelowa jasho akitokea kwenye klabu ya usiku ya Tru mjini Hollywood katika ziara fupi ya matembezi.
Mtengeneza nywele wake Tiffanie Dixon anakumbuka usiku huo alipohojiwa na Vanity Fair, kwamba Whitney alirejea hotelini ambako walisoma naye pamoja Biblia. "Miwani yake ilivunjika hivyo akasoma huku akiwa ameshikilia lenzi moja ndogo," alisema Tiffanie.
Siku aliyofariki, Whitney alipata kifungua kinywa na wanaume watatu wasiofahamika ambao aliwaona siku moja kabla.
Mmoja wa wanaume hao aliliambia Jarida: "Whitney alikuwa akipita akiwa kavalia sweta la kijivu, kofia na miwani ya jua. Alikuwa akinuka pombe.
"Akakaa nasi kwa dakika kumi, alikuwa na bakuli la matunda, akatukumbatia na kuondoka zake."

No comments: