Wafanyakazi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na baadhi ya Maofisa wa Shirika la Viwango nchini (TBS) wakiteketeza pamba bandia katika dampo la Pugu Kinyamwezi jana baada ya shirika hilo kuzikamata Kariakoo jijini.
SHIRIKA la Viwango nchini (TBS) limeteketeza pamba bandia yenye thamani ya dola za Kimarekani 13,200 Dar es Salaam jana baada ya kuikamata kwenye ghala la mmoja wa wafanyabiashara wakubwa Mtaa wa Nyamwezi, eneo la Kariakoo.
Pamba hizo kwa ajili ya matumizi ya vidonda zilizokutwa kwenye maboksi zaidi ya 200 zingeweza kusababisha madhara makubwa kwa wagonjwa kutokana na kutoa kemikali zinazosababisha vijidudu hatari vinavyoshambulia kidonda cha mgonjwa.
Ofisa Habari wa TBS, Roida Andusamile amesema walizikamata mwishoni mwa mwezi uliopita dukani kwa mfanyabisahara huyo zikiwa kwenye hatua za mwisho kwa kuuzwa kwa wateja.
No comments:
Post a Comment