KUTOKA KUSHOTO: Michael Jackson, Matt Fiddes na Randy Jackson.
Mlinzi wa zamani wa Michael Jackson ameibuka na kudai kwamba mwimbaji huyo ni katili mno ambaye aliamuru wafuasi wake wa karibu kumuua mdogo wake, Randy, imefahamika.Katika mahojiano na gazeti moja, mlinzi huyo Matt Fiddes alidai, "Michael Jackson alikuwa akigombana na kaka zake kwa miaka. Walikuwa wakihaha kusaini mkataba unaofikia Dola za Marekani milioni 500 wa ziara ya kundi la Jackson 5."
Fiddes, mtaalamu wa mazoezi ya kujilinda ambaye alifanya kazi na Michael Jackson nchini Uingereza na Marekani alifafanua, "Maji yalifika kichwani wakati Randy alipojaribu kulazimisha kumpita mlinzi ili kwenda kumkabili Mfalme huyo wa Pop ana kwa ana kwenye nyumba moja alikokuwa amepanga. Michael Jackson aliamuru apigwe risasi."
Hata hivyo, hakuna aliyemfyatulia risasi Randy… lakini Fiddes alisema, "Randy aliogopa sana na akachukua simu na kutishia kuviita vyombo vya habari. Aliwaambia walinzi, "Kama mkinifyatulia risasi dunia nzima itajua hilo."
Fiddes aliendelea, "(Michael) alikuwa amelewa dawa na kwa bahati Randy alikuwa na akili zake timamu."

No comments:
Post a Comment