Thursday, May 10, 2012

NDEGE MPYA YA URUSI YAANGUKA NA KUUA ABIRIA WOTE 50...

                                BREAKING NEWS!!                                         
Askari wa Uokoaji wa Indonesia walipokuwa wakisoma ramani ya eneo ilipoanguka ndege ya Urusi juzi.
Waokoaji wa Jakarta, mji ulioko kusini mwa Indonesia wameokota miili kadhaa kwenye eneo ilipoangukia ndege ya Sukhoi Superjet 100 ya Urusi ambayo ilipoteza mawasiliano ya rada wakati ikiruka kwa maonesho ikiwa na abiria 50 juzi. Hakuna waliosalimika katika eneo hilo la milima.
Maofisa wa  Indonesia walijaribu kutembea kwa miguu kwenye miteremko mikali ya milima hiyo na kwa helikopta, lakini hali mbaya ya hewa ilikwamisha zoezi hilo la kusaka miili.
"Kufuatia hali mbaya ya hewa, sikuweza kuruhusu vikosi vya uokoaji kwenda kwenye eneo la ajali na kuamuru virudi kambini," rubani wa helikopta ya uokoaji ya jeshi amewaambia waandishi wa habari leo. 
Wataalamu hatahivyo walifanikiwa kuchukua picha za eneo ilipoanguka ndege hiyo.
Kufuatia ene hilo kutofikika kwa urahisi, miili italazimika kuwekwa kwenye nyavu na kuvutwa kwa kamba na helikopta. Wataalamu wamesema utambuzi wa miili hiyo utachukua muda mrefu kidogo kutokana na kuharibika vibaya.
Mapema leo, Wakala wa Taifa wa Utafiti na Uokoaji walithibitisha kupatikana kwa mabaki ya ndege hiyo.
Urusi inajiandaa kupeleka vikosi viwili vya askari wa uokoaji vya IL-76 na helikopta kwenye eneo la tukio.
Msemaji wa kikosi cha jeshi kilicho jirani na eneo la tukio, Ali Umri Lubis amesema ndege hiyo imekutwa eneo la Cijeruk, jirani na Mlima Salak, karibu kabisa na mji wa Bogor, West Java.
Eneo ilipoanguka ndege hiyo na kuua watu wote 50.

No comments: