JUU: Mahakama ambapo kesi ilisikilizwa. CHINI: Jumba ambalo unyama huo ulikuwa ukifanyika. PICHA NDOGO: Andrew Clappison. KULIA: Linda Clappison akielekea mahakamani kusikiliza hukumu yake.
Mama mmoja ambaye aliwanyanyasa watoto wake wawili na kuwaweka kwenye vyumba vya kulala vilivyokuwa baridi sana hadi mtoto wake mmoja akikaribia kuganda, amehukumiwa kifungo cha miezi 18 jela hivi karibuni.Kwa zaidi ya kipindi cha miaka mitano wamekuwa wakipigwa na kulazimishwa kufanya kazi kwa mikono badala ya kwenda shule, wakioga maji baridi na kufungiwa gizani.
watoto wote walilazimika kulala na nguo zao za ndani tu bila godoro au mashuka katika chumba ambacho hakina mashine za joto, Mahakama kuu ya Hull ilielezwa wakati wa kusikilizwa kesi inayomkabili Linda Clappison.
Hatahivyo, mama huyo mwenye miaka 46 aliweza kuwahadaa wafanyanyakazi wanaokusanya uchafu kwa kutoa nje midoli na mabaki ya vitafunwa vichache wakati wanapokuja kuzoa taka na hivyo 'kuonekana kama familia yenye amani na furaha'.
Kijana Andrew Clappison aliiambia mahakama alikuwa akiishi jehanamu alipokuwa na umri kati ya miaka 10 na 16, na alifikia hatua ya kujaribu kujiua kutokana na mateso hayo.
Binti ambaye sasa ana miaka 13, na ambaye hawezi kutajwa kwa sababu za kisheria, alikumbana na mateso kama hayo akiwa na umri kati ya miaka sita na 11.
Pia alinyolewa nywele zake kichwani mara tano na mama yake na kulazimishwa kusema kuwa alipenda mwenyewe kunyoa 'sababu alitaka afanane na Britney Spears'.
Mama huyo wa watoto wanne, Clappison anayetokea Keyingham, East Yorkshire, alitiwa hatiani kwa makosa ya udhalilishaji watoto mwezi uliopita.
Hatimaye suluhisho likapatikana pale binti huyo alipokwenda shule na kuwaeleza walimu kuwa hataki kurudi nyumbani kwa mama yake.
Alitoa hukumu hiyo, Jaji Michael Mettyear aliwapa pole waathirika hao vijana akiwataja kama 'aina ya watoto ambao kila mzazi angewakubali'.
Alimweleza Clappison: "Jela haiepukiki. Umeharibu maisha ya watoto hawa."
Andrew mwenye miaka 18, aliieleza mahakama wakati alipokuwa na miaka 10 ndipo mama yake alipobadilika baada ya baba yake kuondoka nyumbani kufuatia mama huyo kuwa na mahusiano na mwanaume mwingine.
Kaka yake mkubwa na dada pia waliondoka nyumbani baada ya manyanyaso kuanza.
Alishikiliwa asiende shule kwa karibu nusu ya siku na alipokwenda wakati wa kurudi alifungiwa kwenye chumba chake chenye giza nene.
Andrew anasema mama ayke alimdunda mangumi, kumchapa vibao na kumtandika mateke, akimchapa kwa mkanda wa ngozi na kumbamiza kichwa chake ukutani bila sababu yoyote.
Adhabu mbaya zaidi ilikuwa ni pale alipopewa maji ya baridi na kumriwa ajitupe ndani yake.
Alisema: "Nilikuwa na namuogopa. Nilikuwa nakunywa chai chumbani kwangu. Hakuniacha nishuke chini. Nilikuwa nikifanyiwa kama mbwa."

No comments:
Post a Comment