Tuesday, May 29, 2012

MWIMBAJI MARY J. BLIGE SASA 'AGEUKA TAPELI'...

Taasisi inayomilikiwa na mwimbaji Mary J. Blige inapokea zaidi kuliko kuchangia, hii ni kwamujibu wa benki moja inayodai kuikopesha taasisi hiyo Dola za Kimarekani 250,000 lakini ikaambulia kulipwa Dola za Kimarekani 400 tu.
Imebainika Taasisi ya 'Mary J. Blige and Steve Stoute Foundation For The Advanced Of Women Now' inashitakiwa na Benki ya TD kutokana na mkopo wa Dola za Kimarekani 250,000 ilizokopa tangu Juni, 2011.
Kwa mujibu wa hati ya mashitaka zilizopatikana mapema mwezi huu mjini New York, Taasisi hiyo iliahidi kulipa pesa hizo kabla ya Desemba 2011, lakini ulipofika wakati kulipa pesa hizo taasisi hiyo iliingiza kwenye akaunti kiasi cha Dola za Kimarekani 368.33 pekee.
Benki inadai ilitaka kuhakikishiwa malipo kwa maandishi Februari 7 na 29, lakini haikupata majibu yoyote kutoka kwa taasisi hiyo.
Kesi hii ni moja tu ya mlolongo wa madai mengi yanayoikabili taasisi hiyo. Mwaka 2010 imeshindwa kulipa kodi ya serikali huku pia ikidaiwa na mwanamuziki tangu mwaka 2011 anayedai malipo yake kwa kutumbuiza katika tamasha la kuchangisha fedha akisema ilipofika muda wa kudai chake, taasisi hiyo ikaingia mitini.
Mwakilishi wa Blige alisema, "Mary J. Blige and Steve Stoute Foundation For The Advanced Of Women Now, Inc. (FFAWN) ipo kwenye pilika za kubadili menejimenti yake na makao makuu."
Aliongeza, "Tumebakiwa na jukumu pekee la kusaidia wanawake kuweza kujiamini na ujuzi muhimu kuweza kumudu vipaumbele vyao."

No comments: