Monday, May 14, 2012

MOTO MKUBWA WALIPUKA MICHUANO YA GRAND PRIX HISPANIA...

                   BREAKING NEWS!!               

Michuano ya mbio za magari ya Grand Prix ya Hispania usiku wa kuamkia leo iligeuka vurugu wakati watu 16 walipojeruhiwa vibaya katika moja ya gereji za timu shiriki.
Moto ulilipuka kwenye jukwaa la timu ya Williams muda mfupi baada ya dereva wa Venezuela, Pastor Maldonado kushinda taji la Barcelona ikiwa ni taji la kwanza la grand prix kwa timu ya Uingereza katika miaka minane.
Mfanyakazi mmoja wa timu ya Williams alisafirishwa kwa ndege kupelekwa hospitali ya Barcelona kwa matibabu zaidi baada ya kuungua vibaya wakati wengine watano walipelekwa kwenye hospitali za jirani kutokana na madhara yaliyosababishwa na moshi.
Baabaye watu wengine 10 walitibiwa kwenye kituo cha afya cha Catalunya kufuatia madhara ya moshi kabla ya kuruhusiwa.

No comments: