Wednesday, May 23, 2012

MKONGWE DONNA SUMMER KUZIKWA KWA FARAGHA LEO...

'Malkia wa Disko' Donna Summer anatarajiwa kuzikwa leo kwenye mazishi yatakayofanyika kwa faragha kwenye kanisa moja huko Nashville, Tennessee.
Imeelezwa kwamba kanisa linatarajia waumini kama 1,000 lakini misa hiyo itakuwa kwa ajili ya waalikwa pekee.
Familia imeamua shughuli hiyo iwe faragha…hawataki kuhusisha vyombo vya habari na kwamba wameandaa orodha maalumu ya wageni ikijumuisha marafiki wa karibu na wanafamilia.
Haijafahamika kama marafiki maarufu wa Donna kama watahudhuria, lakini imeelezwa kwamba watu mbalimbali sasa wako safarini kuja kuhudhuria shughuli hiyo.
Donna Summer alifariki dunia mjini Florida wiki iliyopita akisumbuliwa na maradhi ya kansa. Amefariki akiwa na umri wa miaka 63.

No comments: