Wednesday, May 23, 2012

ALIYEMSHAMBULIA HADI KIFO BOYFRIEND WA BINTI YAKE KWENDA JELA...

Mama ambaye alimshambulia hadi kufa rafiki wa kiume wa binti yake mwenye miaka 13 baada ya kuweka picha za utupu za binti yake mtandaoni, anakabiliwa na adhabu ya kifungo jela.
Gedu Bibi mwenye miaka 47, alimshambulia Sumon Miah (pichani) mfanyakazi wa hospitali mwenye miaka 21 nyumbani kwake baada ya kuonesha picha za binti yake ambaye bado ni mwanafunzi.
Mara baada ya kijana huyo kufika nyumbani, Gedu alimtwanga kichwani na mguu wa meza na kuanguka akiwa taabani kuanzia hapo hadi mauti yalipomkuta akiwa bado hajapata fahamu.
Sumon alifariki siku tisa baadaye kutokana na majeraha kwenye ubongo Oktoba 17, 2006.
Gedu alimwambia binti yake awaeleze polisi kwamba alimpiga wakati akijitetea baada ya mpenzi wake huyo kutaka kumchoma na kisu. Mtoto wake wa kiume mwenye miaka 12, Fhalak naye pia alifundishwa kusema hivyo akiulizwa na polisi.
Wapelelezi walimaliza uchunguzi wao mwaka 2008 lakini taarifa za usahihi zimepatikana miaka miwili baadaye ambazo zimepelekea Gedu na mpenzi wake wa zamani anayemiliki mgahawa, Lilu Miah, kushitakiwa kwa mauaji.
Baada ya mashitaka kwenye mahakama ya Old Bailey, wazee wa baraza walimfutia Gedu mashitaka za mauaji lakini wakamtia hatiani kwa kuua bila kukusudia. Lilu Miah alifutiwa hatia zote za mauaji na kuua bila kukusudia.
Gedu, ambaye alidai kuwa alikuwa amelala wakati wa shambulio hilo, alishinikiza kwamba mume wake Angur Miah kuwa anahusika.
Jaji Gerard Gordon alisema atamhukumu Gedu katika tarehe za mbele wakati ushauri utakapopatikana.
Mahakama ilielezwa Sumon Miah na Shuhina Khanam walianza mahusiano ya kimapenzi baada ya kukutana hospitalini ambako alikuwa akifanya kazi kama mbeba mizigo wakati binti huyo alikwenda kumtembelea rafiki yake.
Siku chache kabla ya shambulio, Lilu Miah alimuonesha Gedu picha nne za binti yake alizozitoa kwenye mtandao.
Oktoba 8, 2006, alialikwa kwenye nyumba ya familia ya Gedu iliyoko Walthamstow.
Baada ya kuwa ameangushwa na mguu wa meza, wakati huohuo silaha hiyo ikafutwa vizuri na kukamatishwa kwa Shuhina kuhakikisha kwamba inakuwa na alama za vidole.
Hakuna damu wala nywele zilizokutwa kwenye silaha, na zilionekana pekee katika kisu anachodai Miah alitumia kumtishia.
Kufuatia kifo cha Sumon, rafiki alikabidhi kamera ya simu kwa polisi, ikiwa na picha zilezile zikiwa zimehifadhiwa kwenye kumbukumbu ndani yake.

No comments: