JUU: Robert akiwa na Mary. CHINI: Jumba ambamo Mary alikutwa amekufa.
Mke wa Robert F. Kennedy Jr. waliyetengana naye amefariki dunia.
Vyanzo vya habari vya kisheria vimeeleza kuwa, Mary Kennedy mwenye miaka 52 alikutwa mchana amekufa kwenye nyumba yake iliyoko Mount Kisco, jijini New York.
Idara ya Polisi wa Bedford walifika eneo la tukio majira ya saa 7:36 kuchunguza sababu za kifo hicho ambacho hakikushuhudiwa na yeyote.
Mary na Robert walioana mwaka 1994. Robert alifungua madai ya talaka Mei, 2010. Mary alikuwa mke wa pili wa Robert. Wanandoa hao walifanikiwa kupata watoto wanne.
Kuna taarifa kwamba Robert F. Kennedy Jr. kwa sasa yuko kwenye mahusiano na Cheryl Hines.
Siku tatu baada ya Robert kufungua madai ya talaka mwaka 2010, Mary alikamatwa kwa kosa la kuendesha gari huku akiwa amelewa.
Msemaji wa familia ya Mary ametoa taarifa akidai, "Tunasikitika mno kwa kifo cha dada yetu mpendwa Mary, ambaye roho yake ya kijasiri na ubunifu itakosekana kwa wote waliompenda. Mioyo yetu inaelekea kwa watoto ambao aliwapenda kuliko chochote."
Taarifa zaidi zinasema kuwa Mary Kennedy kisheria alikuwa bado ni mke wa Robert Kennedy Jr. hadi mauti yalipomfika.
Robert alifungua madai ya talaka mahakamani, lakini kwa mujibu wa kumbukumbu za mahakama, mchakato wa shauri la madai hayo ya talaka lilikuwa bado likiendelea na Jaji alikuwa hajatoa uamuzi kuhitimisha.

No comments:
Post a Comment