Mchungaji Marvin Winans, mtu aliyeongoza shughuli ya msiba wa Whitney Houston kisheria hakutakiwa kuendesha gari wakati alipoporwa gari lake wiki iliyopita sababu leseni yake ilikuwa imefungwa.
Kwa kifupi, Winans ni mtu anayesakwa huku waraka wa mahakama wa kukamatwa ukiwa bado haujaisha muda wake, hii ni kwa mujibu wa vyanzo vya habari.
Marvin ambaye familia yake ni waimbaji wakongwe wa muziki wa injili, aliripotiwa kupoteza sifa zake za kuendesha gari tangu Mei 9, mwaka huu baada ya kushindwa kulipa faini mbili Desemba mwaka jana. Moja kwa kuwalaghai askari wa usalama barabarani na nyingine kwa kutumia leseni iliyokwisha muda wake.
Baada ya kushindwa kutokea mahakamani, Jaji alitoa waraka wa kukamatwa Winans Mei 15, siku moja kabla ya kuporwa gari lake kwenye kituo cha mafuta huko Detroit.
Winans alivieleza vyombo vya habari kuwa, "Tukio hilo linashughulikiwa na timu yake ya utawala, na si yeye."
Cha kushangaza ni kwamba, Winans amepigwa faini mara 11 tangu mwaka 2009.

No comments:
Post a Comment