Saturday, May 26, 2012

CHEKA TARATIBU...

Baada ya kukerwa sana na wazazi wake waliokuwa wakimlazimisha asome kwa bidii, kijana mmoja kaamua kunywa sumu ili aondokane na kero hiyo. Kwa bahati baada tu ya kumeza sumu akawahiwa na mama yake kwa kupatiwa maziwa na kukimbizwa hospitali huku akiwa hana fahamu. Alipozinduka huku akiamini kwamba amekufa, akawaona wazazi wake wakiwa wamemzingira kitandani. Kijana akaropoka kwa ukali, "Mmenifuata hadi huku ahera? Sikubali bora nirudi duniani!" Akatimua mbio kuelekea nje! Duh! Ama kweli usilolijua...

No comments: