Sunday, May 13, 2012

MAMA AJIVUNIA SURA YA KUCHEKESHA YA MWANAE...


Mama ambaye mtoto wake wa kiume alizaliwa na mapungufu kadhaa yaliyomsababishia kukosa macho ametoa video ya kusisimua akiweka wazi magumu aliyopitia na jinsi mtoto wake huyo wa kiume anavyozikabili changamoto kutokana na muonekano wake wa kuchekesha.
Katika video hiyo aliyoisambaza kwenye mtandao wa YouTube, Lacey Buchanan anayetokea Woodbury, huko Tennessee, anaonekana akionesha kadi kadhaa jinsi alivyobeba mimba na maoni mbalimbali yaliyofuatia baada ya kumzaa kijana wake, Christian.
Ndani ya filamu hiyo yenye urefu wa dakika saba, anaonekana amembeba kifuani Christian mwenye mwaka mmoja sasa akimuanika sura yake kwenye kamera mwishoni mwa video huku akimbusu na kuonyesha fahari anayojisikia kuwa naye.

No comments: