Sunday, May 13, 2012

CHEKA TARATIBU...

Dereva mmoja anayefanya kazi nyumbani kwa fisadi mmoja mjini Mwanza kajikuta kwenye wakati mgumu baada ya kumpa ujauzito binti wa bosi wake.
Katika kutafuta namna ya kuepuka adhabu kali kutoka kwa baba wa binti huyo, Dereva huyo akapata wazo la kwenda kwa mganga mmoja maeneo ya Nyamagana ili kupoteza ushahidi.
Alipofika kwa mganga akamweleza yaliyomsibu na kwamba kesho yake ataitwa mbele ya bosi wake huyo kujitetea. Mganga huyo maarufu akamjibu kuwa ni tatizo dogo sana na kwamba atafanya 'ndumba' zake na kupoteza sehemu za siri za Dereva huyo jambo ambalo aliliafiki mia kwa mia.
Siku ya kujitetea mbele ya bosi wake ikafika ndipo Dereva akaanza kujitetea, "Bosi, mie sihusiki na ujauzito huo." Bosi kwa ukali akasema, "Hivihivi tu? Hebu thibitisha!" Ndipo Dereva akavua suruali yake, kwa mshangao hakuwa na sehemu za siri! Watu wote wakabaki wanashangaa...
Kesho yake jamaa kadamkia kwa mganga. Akiwa njiani akawa akipishana na kinamama wakitoka na wengine wakielekea nyumbani kwa mganga huku wamejifunika khanga wakilia. Alipofika nyumbani akakuta watu kibao na kila dalili kuwa kuna msiba. Akachanganyikiwa kusikia watu wakiongea na wengine kulia huku wakionesha kutoamini kifo cha mganga. Hapo jamaa kama kichaa akaanza kuvamia kila mtu na kuuliza bila mafanikio, "Samahani, poleni kwa msiba. Vipi mganga hakuacha kamzigo kangu?" Hatimaye mpaka Dereva akaamua kukubali matokeo na kubaki akijutia nafsi yake...

No comments: