Wednesday, May 2, 2012

MAKONGORO MAHANGA ASHINDA KESI

                  BREAKING NEWS!!              
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa Mbunge wa Segerea (CCM), Dk. Milton Makongoro Mahanga mchana huu ameshinda kesi iliyokuwa ikipinga matokeo yaliyompa ushindi katika uchaguzi mkuu uliopita. Kesi ilifunguliwa na mgombea ubunge kwa tiketi ya  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Fred Mpendazoe, Novemba mwaka jana, aliyeiomba mahakama itengue matokeo hayo kwa vile kulikuwa na kasoro kadhaa katika uchaguzi huo. Mbali na Mahanga aliyekuwa akitetewa na wakili wa kujitegemea, Jerome Msemwa, wadaiwa wengine walikuwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na aliyekuwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Segerea.

No comments: