Wednesday, May 30, 2012

LADY MADONNA AUPONDA WIMBO WA LADY GAGA...


Mwimbaji mashuhuri duniani, Lady Madonna alipiga wimbo wa Lady Gaga uitwao "Born This Way" wakati wa mazoezi kujiandaa kwa tamasha mjini Tel Aviv, nchini Israel.
Madonna hakufanya hivyo kwa nia nzuri bali alitaka kukumbushia mashabiki wake madai kwamba wimbo huo ni marudio aliyofanya Lady Gaga kutoka katika wimbo wa Madonna uitwao "Express Youself".
Wakati wimbo wa "Born This Way" ukiingizwa mitaani, Madonna aliuponda hadharani akiita kuwa ni 'marudio ya kushangaza' ya wimbo wake wa 'Express Youself' kisha kuuita usiokuwa na maana.
Upande wake, Lady Gaga ameita maoni ya Madonna kuwa 'yamepitwa na wakati'.

No comments: