Wajinga wawili Juma na Jeba walikuwa wakichimba mtaro wakati wa jua kali sana. Juma akamwambia mwenzake, "Kwanini sisi tuko hapa kwenye mtaro wakati bosi wetu kajificha kwenye kivuli cha mti?" Jeba akajibu, "Sijui bwana." Juma akasema, "Nakwenda kumuuliza."
Akaenda moja kwa moja kwa bosi wake na kuuliza, "Kwanini sisi tunachimba mtaro juani wakti wewe umejificha hapa kivulini?" Bosi akajibu, "Werevu." Juma akauliza, "Unamaanisha nini Werevu?" Bosi akasema, "Vizuri, nitakuonesha. Nitaweka mkono wangu kwenye mti huu nataka upige ngumi kwa nguvu zako zote." Juma akavuta kasi na kurusha ngumi kwa nguvu akijaribu kupiga mkono wa bosi. Yule bosi akaondoa mkono wake pale na ngumi ya Juma ikatua kwenye mti. Kisha bosi akasema, "Huu ndio Werevu!"
Juma akarudi kwa mwenzake. Jeba kamuuliza, "Kasemaje?" Juma akajibu, "Kasema tupo hapa juani sababu ya Werevu." Jeba akauliza, "Werevu ndio nini?" Juma akajiziba uso wake kwa mikono na kusema, "Chukua chepeo lako halafu piga mikono yangu hapa kwa nguvu zako zote!" Duh… hebu pata picha kilichotokea. Ama kweli ujinga gharama...

No comments:
Post a Comment