BREAKING NEWS!!
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam mchana huu imemthibitisha rasmi John Mnyika kuwa Mbunge halali wa Jimbo la Ubungo baada ya kushinda kesi yake ya kupinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika mwaka 2010 iliyofunguliwa na mpinzani wake, Hawa Nghumbi wa Chama cha Mapinduzi (CCM).Mnyika alishinda ubunge wa Jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Mahakama hiyo pia imemuamuru mlalamikaji, Nghumbi kulipa gharama zote za kuendesha kesi hiyo.
Mara baada ya hukumu kutolewa, yalilipuka mayowe na vifijo kutoka kwa wanaoaminika kuwa wafuasi wa Chadema na mashabiki wa Mbunge huyo kijana machachari aliyejizolea umaarufu mkubwa bungeni.

No comments:
Post a Comment