Saturday, May 26, 2012

CHRIS JERICHO ASIMAMISHWA MIELEKA YA WWE...



Pambano la mieleka la WWE nchini Brazili liliingia doa juzi pale wanaosimamia sheria walipoingilia kati na kusimamisha pambano na kutishia kumkamata Chris Jericho kwa kuidhalilisha bendera ya Brazili.
Tukio hilo lilitokea wakati wa pambano kati ya Jericho na C.M. Punk ambaye alikuwa akipepea bendera kwenye ulingo.
Jericho akaipora bendera na kuikunja na kuitupa chini kabla ya kuipiga teke hadi nje ya ulingo, kitendo kilichowakera polisi na kuingia ulingoni kisha kusimamisha pambano hilo.
Imeelezwa Jericho alionywa kudhalilisha bendera ya taifa ni kosa la jinai nchini Brazil.
Polisi walimpa nafasi Jericho ya kuomba radhi umati uliohudhuria ama kwenda jela. Jericho akachukua kipaza sauti na kuwaambia mashabiki kwamba papo hapo anaomba radhi kwa kitendo alichofanya. Hapo ndipo polisi wakaruhusu pambano hilo kuendelea.
Vyanzo vya habari vyenye ukaribu na WWE vimesema kukunjwa na kutupwa bendera hiyo hakukupangwa au kupewa ruksa na maofisa wa WWE.
WWE imetoa tamko rasmi ikisema, "Chris Jericho amesimamishwa kwa muda usiojulikana kwa kitendo chake cha utovu wa nidhamu kudhalilisha bendera ya Brazil katika pambano la WWE mjini Sao Paulo lililofanyika Mei 24, mwaka huu. WWE inaomba radhi kwa raia na serikali ya Brazili kwa tukio hilo."

No comments: