Tuesday, May 22, 2012

CHEKA TARATIBU...

Baada ya kukurupushwa akiwa kasimama na mke wa mtu, jamaa akaamua kujisalimisha kwa kujificha juu ya mti. Mume wa mwanamke yule baada ya kumtafuta sana kaamua kupumzika chini ya mti ule ule aliojificha yule jamaa. Mara akapita rafiki wa yule mume na kuanza kumsimulia mkasa mzima. Kwa hasira yule mume akaendelea kusimulia, "Haki ya mungu ana bahati sana, yaani sikubali lazima niue mtu leo. Bwana uliye juu unisamehe." Akimaanisha Mwenyezi Mungu. Kusikia vile huku akitetemeka akidhani ameonekana, jamaa aliyejificha juu ya mti si akashuka, "Mie nimeshakusamehe kitambo ila nihakikishie kama na wewe umenisamehe..! Unaambiwa kila mtu akatimua mbio kivyake kwa mshituko...

No comments: