Jamaa katimka alfajiri kwenda kumuona dokta hospitalini. Alipofika kabla ya salamu akaanza kujieleza shida yake, "Dokta, nahitaji msaada wako. Mke wangu anafikiria kuwa mimi ni kuku!" Dokta akauliza, "Kwa muda gani sasa anakufikiria hivyo?" Jamaa akajibu, "Miaka miwili sasa!" Dokta akauliza tena, "Sasa kwanini imekuchukua muda mrefu hivyo bila kuja kuniona?" Jamaa akajibu, "Tulikuwa tunahitaji mayai." Duh, uchizi mwingine bwana...

No comments:
Post a Comment