Monday, May 14, 2012

ALIYEKUWA AKISUBIRI KUZIKWA 'AFUFUKA'...

Waombolezaji katika msiba nchini Misri walibubujikwa na machozi ya furaha baada ya 'marehemu' waliyekuwa wakimzika kuamka.
Hamdi Hafez al-Nubdi mwenye miaka 28 aliyekuwa akifanya kazi ya uhudumu kutoka Naga al-Simmanm, karibu na Luxor alitangazwa amekufa baada ya kupata shinikizo la moyo akiwa kazini.
Mwili wake ulikuwa ukiandaliwa kwa ajili ya mazishi wakati daktari akipelekewa kusaini cheti cha kifo, ndipo ikagundulika kwamba bado alikuwa na joto.
Wanafamilia walishaamini kabisa kuwa al-Nubdi amekufa na walikuwa tayari wameosha mwili wake, kwa mujibu wa utamaduni wa Kiislamu, na walikuwa wakijiandaa kwa mazishi yake Ijumaa jioni.
Baada ya kugundua alikuwa bado na joto, daktari alimpima na kugundua kuwa bado anapumua.
Haraka akamrudisha al-Nubdi wodini sambamba na mama yake ambaye alizirai baada ya kusikia kijana wake yu hai.
Baada ya kufuta shughuli ya mazishi, waombolezaji walianza kusherehekea 'kufufuka' kwa al-Nubdi.
Si mara ya kwanza kwa mtu 'kufufuka' kwenye msiba.
Mwezi mmoja tu uliopita, kikongwe wa Kichina mwenye miaka 95 alitoka kwenye jeneza lake ikiwa ni siku sita tu tangu adhaniwe kuwa amekufa.
Li Xiufeng alikutwa na na jirani yake amelala kitandani huku akiwa hapumui wiki mbili baada ya kuanguka na kupata majeraha kichwani nyumbani kwake Beiliu, Jimbo la Guangxi.
Wakati jirani alipoona hawezi kumuinua mstaafu huyo, wakahofia mabaya na kudhani kwamba kikongwe huyo ameshafariki.
Aliingizwa kwenye jeneza ambalo lilihifadhiwa nyumbani bia kufunikwa kwa mujibu wa utamaduni wa Kichina kwa ajili ndugu na jamaa kutoa heshima zao za mwisho.
Lakini siku moja kabla ya mazishi, majirani walikuwa jeneza hilo likiwa tupu na baadaye wakamuona kikongwe huyo ambaye hakuwahi kuinuka hapo kabla, akiwa jikoni kwake anapika.

No comments: