Saturday, May 12, 2012

CHEKA TARATIBU...

Mwanamke mmoja asiyependa kupitwa na kitu kamuona mchungaji wa kanisa jirani akiingia chumbani kwa mpangaji mwenzake maeneo ya Tandale Uzuri.
Kesho yake asubuhi wakiwa uani wanafua akamuuliza mwenzake, "Shosti nimeona jana mchungaji anaingia kwako, vipi alikuja kukuombea?"
Kuonesha hakupenda kufuatiliwa yule mwenzake akamjibu kwa kufoka, "Acha umbea! Mbona kwako kila siku anaingia mwanajeshi, kwani kuna vita?" Duh, uswahilini kuna mambo...

No comments: