Mmasai mmoja kutoka kijijini kwa mara ya kwanza anapata nafasi ya kuvaa nguo ya ndani alipofika mjini. Inaaminika kwamba wengi wao wa kabila hilo, hasa wale wanaofuata mila huwa hawana mazoea hayo. Basi bwana, safari ya kurudi kwao ikawadia na yule Mmasai akatinga nguo yake ya ndani na kuanza safari huku akipewa tahadhari na mwenyeji wake kuwa awe makini maeneo ya Chalinze kuna vibaka sana. Safari ikaanza na akiwa njiani si akabanwa na haja... Akamuomba dereva asimamishe gari ili apate kujisaidia maeneo ya Chalinze. Kwakuwa si asili yake kuvaa nguo ya ndani, jamaa akafunua shuka lake na kuanza kujisadia. Alipomaliza akainuka na kupata mshangao wa mwaka na kupiga kelele, "Eyooouwiii, hii mutu ya Chalinse inakwiba hata kinyesi! Kweli sina hamu...!"

No comments:
Post a Comment