Tuesday, May 8, 2012

CHEKA TARATIBU...

Jamaa mmoja baada ya kuzidiwa na kilevi kaamua kulala kwenye mtaro. Usiku wa manane askari aliyekuwa doria akamkuta jamaa hajitambui. Baada ya kujaribu kumwamsha zaidi ya nusu saa ikiwa pamoja na kupiga virungu kadhaa, hatimaye jamaa akazinduka. Ndipo askari akamwambia, "Nakupeleka kituoni kwa kosa la kulewa kupita kiasi." Yule mlevi akamjibu, "Askari, una uhakika kwamba nimelewa?" Askari akasisitiza, "Ndio, nina uhakika umelewa!" Yule mlevi akainuka na kushangilia kwa sauti, "Duh, kweli Mungu mkubwa. Nilijua nimekufa afande!" Askari akabaki kaduwaa...

No comments: