Monday, May 7, 2012

CHEKA TARATIBU...

Ndugu wako msibani wakilia kwa uchungu baada ya kumpoteza mzee wao. Huku kila mmoja akitamka yake ya moyoni, ghafla kwa huruma akatokea mtoa roho za watu mbele yao. Kwa upole akasema, "Nimeguswa mno kwa jinsi mlivyokuwa mkilia. Si kawaida yangu kuwa na huruma nichukuapo roho ya mtu." Wakati wote wakiwa kimya kwa mshangao, ndipo mtoa roho akauliza, "Nimesikia kilio chenu hivyo namrudishia uhai mzee wenu. Kwakuwa sitakiwi kuondoka hivi hivi, je nichukue roho ya nani kati yenu?" Duh, jamaa kusikia hivyo wakatazamana usoni kisha kila mmoja kutimua mbio kwa njia yake! Ama kweli maisha matamu...!

No comments: