Jamaa walikuwa wakisafiri katika pick-up yao wakitokea mnadani mkoani Singida. Wakiwa njiani dereva akaona tawi ya mti likining'inia njiani na kwa kujua kwamba linaweza kuwadhuru wenzake wa nyuma akatoa tahadhari, "Inama." (Kwa Singida neno Inama linamaanisha Nyama). Kwa uroho wao, jamaa kusikia vile badala ya kuinama wakaendelea kusimama huku sasa wakiangaza huku na kule. Punde wote wakajibamiza kwenye lile tawi na kuanguka kama mizigo. Duh...

No comments:
Post a Comment