Monday, May 21, 2012

BEHEWA KUUKUU LAGEUKA JUMBA YA KIFAHARI...

Ukizungumzia ujenzi wa jumba la starehe, basi huwezi kuacha kumtaja Jim Higgins.
Meneja Usafiri huyo mstaafu mwenye miaka 60, ameibuka kuwa mmoja wa wenye nyumba za kipekee nchini Uingereza, kufuatia jumba lake lililojengwa kuzingira behewa wa treni lililotelekezwa juu ya reli.
Jumba hilo lililopo Ashton, mjini Cornwall, limenakshiwa na kundelea kuhifadhi kumbukumbu ya behewa lenye umri wa miaka 130 la reli ya zamani ya Great Western kwenye kuta za jumba hilo.
Higgins ambaye asili yake ni Buckinghamshire alichukua jumba hilo kutoka kwa aliyekuwa baba mkwe wake Charles Allen ambapo alilazimika kujenga kwa kuzingira behewa hilo kutokana na sheria za mipango miji kutoruhusu behewa hilo kuhamishwa.
Higgins anasema, "Behewa hilo alikuwa akiishi mwanamke mmoja Elizabeth Richards miaka ya 1930.
"Lilifahamika kama Lizzies Place hadi alipofariki mwaka 1966.
"Kisha lilibaki tupu kwa miaka kadhaa hadi aliyekuwa mkwe wangu alipotafuta sehemu ya kukaa baada ya kustaafu.
"Alikuwa fundi seremala mzuri na alikuwa akitafuta kibali cha kujenga makazi ya kuishi baada ya kustaafu.
"Alifika akitokea Middlesex na kutokea kupenda mahali behewa hilo lilipokuwa."
Lakini Higgins alipoomba kibali cha kujenga jumba akaambiwa behewa hilo lipo mahali hapo kwa miaka mingi sana hivyo ni 'haki za babu.'
"Halikuweza kuhamishika. Hivyo akaamua kujenga kwa kulizingira.

No comments: