Picha mbalimbali za Pusepa baada ya kukamatwa na Polisi. Picha ndogo mbili chini: Alec na Pusepa.
Mwanamke mmoja amekamatwa kwa tuhuma za kujaribu kuua akidaiwa kumchoma visu mchumba wake katika mzozo mkali kati yao siku ya Ijumaa asubuhi.Yekaterina Pusepa alikutwa akibubujikwa machozi eneo la tukio huku akiwa amevalia fulana yake nyeupe, suruali ya jeans na mikononi akiwa ametapakaa damu iliyotokana na majeraha ya mpenzi wake, Alec Katsnelson.
Alionekana pichani alipokuwa kando ya njia pembezoni mwa nyumba yake iliyoko mjini New York kabla ya kuondolewa eneo hilo chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Askari polisi kadhaa waliitwa baada ya wapenzi hao kulumbana kwa sauti na kuwabugudhi majirani majira ya usiku.
Pusepa alifikishwa mahakamani Jumamosi ambako alisomewa mashitaka ya kujaribu kuuana shitaka la pili la kudhuru mwili, lakini hakutakiwa kujibu chochote.
Pusepa mwenye miaka 22, anatuhumiwa kumchoma kwa kisu cha jikoni Katsnelson ambaye pia ana miaka 22 kwenye makazi yao wanayochangia na binamu yake huko Manhattan wakati wa mabishano yaliyowaamsha majirani.
Jirani mmoja alisema: "Alikuwa akilalama kwa sauti.
"Yalikuwa maneno makali ya hasira kama mtu aliyekuwa akitoa vitisho. Unaweza kusema kulikuwa na mapigano."
Pusepa alisikika akipiga kelele 'Piga simu 911', akimweleza opereta: "Kuna mtu anachuruzika damu mtaani - inaonekana kapigwa risasi ama kachomwa kisu!"
Kisha akakokota mwili wake hadi ghorofa ya chini mtaani ambako aliulalia juu yake.
Mtuhumiwa amedai kuwa majeraha hayo yametokana na kujidhuru mwenyewe, akisema alichukua kisu katikati ya mapambano yao lakini ghafla mpenzi wake huyo akampora na kujichoma nacho kifuani.
Vyanzo vya habari vimeeleza kwamba maelezo ya Pusepa sio kweli na kuwa amebadili stori katika maelezo yake baada ya kukamatwa majira ya Saa 9 alfajiri.
Wapenzi hao walianza urafiki wao Novemba mwaka jana na kwamba wamekuwa na urafiki wenye utata mkubwa.
Kuna wakati Katsnelson alijaribu kumtimua Pusepa, hali iliyozusha ugomvi uliomsababishia kukaa jela kwa wikiendi moja.

No comments:
Post a Comment