Monday, April 16, 2012

NICKI MINAJ ADAI HADHARANI BABA YAKE ALITAKA KUMUUA UTOTONI...

Baba wa mwimbaji Nicki Minaj ameibuka na kudai kusikitishwa na kuumizwa na taarifa za hivi karibuni kwamba alitaka kumuua binti yake huyo wakati wa utotoni, na kwamba ametokeza hadharani kutaka dunia ielewe kuwa yeye ni mtu safi na si mnyama kiasi hicho.
Katika mahojiano aliyofanya Nicki kwenye kipindi cha "Nightline" hivi karibuni, alimshambulia baba yake, Omar akimtaja kuwa muathirika wa dawa za kulevya na mlevi ambaye alifikia kutishia kumuua mama yake na hata kuteketeza kabisa kwa moto nyumba yao.
Nicki alisema, "Nilitaka kumuua (Baba). Nilitamani kama angekuwa amekufa..."Tulikuwa tukihofia maisha ya mama yangu sababu popote alipokutana naye alitishia kumuua."
Lakini vyanzo vya habari kutoka familia hiyo vimeeleza, madai hayo aliyotoa Nicki yametiwa chumvi mno...Omar amekiri kuwa na matukio ya kuchukiza wakati Nicki akiwa mtoto...lakini amesisitiza hakufikia kiwango alichokisema Nicki kwenye mahojiano hayo.
Vyanzo viliendelea kusema, Omar hakujua kama Nicki amefikia kuwa na hisia kiasi hicho dhidi yake, na kwamba angeamua kwenda kumshambulia katika mahojiano yaliyorushwa moja kwa moja hewani kwenye vyombo vya habari.
Imeelezwa kuwa baba yake bado anampenda sana Nicki...na ataendelea kumpenda.

No comments: