Monday, April 16, 2012

CHEKA TARATIBU...

Mzee mmoja kaingia baa huku akiwa amevalia jezi ikiwa imeandikwa Namba 12 kubwa kifuani. Baada ya kusubiri kwa zaidi ya masaa mawili bila kuhudumiwa ndipo alipoamua kumuita kwa sauti meneja wa baa ile na kuuliza, "Kwanini wahudumu wako wananikodolea macho na kunipita bila kunihudumia?" Meneja akajibu, "Ni kweli, hatuwezi kukuhudumia." Mzee kwa ukali na sauti ya juu akahoji, "Kwanini?" Meneja akajibu, "Hujafikisha miaka 18!" Duh, jichungeni na mavazi yenu jamani...

No comments: