BREAKING NEWS
Mwimbaji wa bendi na mcharaza drum mahiri Levon Helm aliyewahi kutamba kwa vibao vyake kama "The Weight" ("Take a load off Annie"...) amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu saratani ya koo.
Helm ambaye aligundulika kuwa na maradhi hayo mwishoni mwa miaka ya 1990, amefariki usiku wa kuamkia leo jijini New York huku akiwa amezungukwa na marafiki na wanamuziki wenzake kitandani.
Helm alianzisha kundi ambalo baadaye likashamiri na kuwa bendi akishirikiana na Robbie Robertson, Richard Manuel, Rick Danko na Garth Hudson mwaka 1964.
Kundi hilo lilipitia majina mengi lakini halikuweza kuwa bendi kamili hadi baada ya ziara waliyofanya na Bob Dylan mwaka 1965 na 1966.
Helm ameshinda Tuzo tatu za Grammy kwa kazi zake binafsi katika miaka minne ya mwisho. Mwaka 2008, bendi hiyo ilipokea Tuzo ya Grammy kwa Mafanikio ya Jumla.
Helm aliyefariki akiwa na miaka 71, ameacha mke na mtoto mmoja wa kike.

No comments:
Post a Comment