Mtoto wa miaka kumi amekuwa akilazimishwa kulala kwenye chumba kidogo kichafu cha kukokea moto kila siku usiku kwa zaidi ya mwaka.
Mama wa mtoto huyo na mpenzi wake walimfungia katika chumba kilichokuwa kikitumika kukokea moto chenye godoro lenye matope, blanketi chafu na kopo kwa ajili ya kujisaidia.
Wapenzi hao, ambao hawakuweza kutajwa majina yao kwa sababu za kisheria, wanakabiliwa na kifungo baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la unyanyasaji watoto kwa makusudi.
Mtuhumiwa wao alihudhuria shule lakini usiku alitelekezwa kwenye baridi na kufungiwa kijichumba nje ya nyumba bila huduma ya choo, mswaki wala vifaa vya kuogea.
Angeweza kufungiwa kwa kipindi kirefu zaidi kama angekutwa anachukua chakula kwenye jokofu nyakati za mchana.
Mateso na maisha magumu ya mtoto huyo yalifichuka pale walimu wa shuleni kwake walipolivalia njuga suala hilo baada ya kuona hali mbaya ya mtoto huyo na ndipo walipoziarifu mamlaka husika.
Alipohojiwa na polisi, mtoto huyo alieleza: "Nilikuwa kama naishi kwenye boksi."
Maofisa wanaochunguza kesi hiyo walifafanua kuwa wapenzi walimfanya mtoto huyo kama 'mnyama'.
Mpelelezi wa Polisi, Konstebo Matt Normanton kutoka kituo cha Blackpool alisema: "Mtoto alikutwa amefungiwa kwenye kichumba cha kukokea moto, akiishi kwa shida, katika hali isiyokuwa ya kibinadamu."
"Sijawahi kuona tukio kama hili kabla - sehemu ilikuwa mbaya kuzidi ya polisi au selo ya mfungwa." Natumaini sitakuja kuona tena tukio kama hili.
"Kulikuwa zaidi kuna shuka moja na kopo kwa ajili ya kujisaidia lililokuwa limejaa mkojo huku ukuta ukiwa na mikwaruzo. Ilikuwa ni 'unyama'.
Aliendelea: "Hakukuwa na hewa, kulikuwa pachafu na baridi. Kulikuwa na dirisha kwa mbali upande wa kulia ambalo limefungwa kabisa na taa moja ya balbu. Palikuwa pia na bakuli lililokuwa na mabaki ya chakula kilichoharibika ndani yake. Kwa kifupi alikuwa kama mfungwa."
Kuhusu mama wa mtoto huyo na mpenzi wake, alisema: "Walikuwa wamekaa sebuleni wakitazama televisheni, wakati mtoto akiwa 'bandani' mwake huku kufuli likining'inia mlangoni.
Banda hilo la mkaa limejengwa kando ya nyumba ya halmashauri wanayoishi wapenzi hao mjini Blackpool.
Ukuta wa ndani ulivunjwa ili kupata nafasi kuweza kuingia kwenye 'banda' alilokuwa akiishi mtoto huyo ambalo mlango wake ulifungwa na makufuli.
Baada ya afya ya mtoto huyo kubainika, alipatiwa matibabu na kukabidhiwa chini ya uangalizi wa serikali ya mtaa.
Sasa anajifagilia kwa maofisa wa serikali ya mtaa kwamba amepiga mswaki kwa mara ya kwanza na kucheza bustanini kama watoto wengine.
Wapelelezi wanasema wapenzi hao wamekuwa wakirudiarudia kumshutumu mtoto huyo wakisema tabia yake hairekebishiki. Wangemfungia kwa kipindi kirefu ikiwa ni nyongeza ya adhabu endapo angejaribu kuchukua chakula kwenye jokofu - nyamba mbichi na vipande vya jibini.
Wapenzi hao ambao hawakupatikana na hatia ya kudhuru mtoto kwa maana ya kuumiza ama kujeruhi, wanatarajia kuhukumiwa mwezi ujao katika Mahakama ya Preston. Jaji Anthony Russell amewatahadharisha kwamba wanakabiliwa na kifungo.
Mama wa mtoto, anayekaribia kufika miaka 30 na mpenzi wake miaka 40, wamezuiwa kumkaribia mtoto huyo.
Kwa kuongezea, hawatakiwi kujihusisha na mtoto yeyote aliye chini ya miaka 16 bila idhini ya mamlaka za jamii.
Madai dhidi ya mtoto huyo mwenye miaka 10, yaliripotiwa kwa mara ya kwanza Kitengo cha Polisi cha Kulinda Watoto Blackpool mwaka jana. Mama yake na mpenzi wake wamedaiwa kumtesa mtoto huyo kati ya Januari 1, 2010 na Januari 25, 2011.
Jirani katika kikao cha Halmashauri alisema: "Kuna ukuta mrefu kati yetu na wao hivyo kushindwa kujua kinachoendelea. Zamani nyumba zote hizi zilikuwa na kijisehemu cha kukokea moto lakini vikaja kuwa havina kazi baada ya kuwekewa heater.
V"Vingi vilibomolewa."
"Hatuelewi kwanini mamlaka husika zimechukua muda mrefu sana kukubali kwamba kuna kitu kibaya kinachoendelea. Inatakiwa ichunguzwe."
Msemaji wa Halmashauri ya Blackpool amesema ripoti kamili kuhusu kesi hii inaandaliwa."

No comments:
Post a Comment