Waumini wakiwa kanisani, mara akatokea shetani madhabahuni! Kila mmoja mle ndani akaanza kutimua mbio huku akipiga mayowe kuelekea mlangoni. Punde kanisa likabaki tupu isipokuwa jamaa mmoja aliyekuwa ameketi kimya. Hilo lilimchanganya kidogo shetani. Akamwendea yule jamaa na kusema, "Haloo, hujui mimi ni nani?" Jamaa akajibu, "Ndiyo, nakufahamu." Shetani akasema, "Vizuri, sasa ina maana huniogopi?" Jamaa akajibu, "Sikuogopi." Shetani akauliza tena, "Na kwanini huniogopi?" Jamaa akajibu kwa kujiamini, "Unajua, nimemuoa dada yako kwa miaka 25 sasa!" Balaa...

No comments:
Post a Comment