Mtoto mmoja katumwa dukani kununua sabuni. Ili asisahau alichotumwa, akabuni mbinu ya kuimba kile alichotumwa, "Sabuni, Sabuni, Sabuni..." Kwa bahati mbaya akiwa njiani akasimamishwa na mzee mmoja. "We mtoto mbona husalimii wakubwa," alifoka mzee huyo. Kwa hofu kubwa yule mtoto akajibu, "Samahani babu, Shikamoo!" Baada ya kujibu na kuondoka, yule mtoto akaanza tena kuimba, "Shikamoo, Shikamoo, Shikamoo..." Kaazi kweli kweli!

No comments:
Post a Comment