Friday, April 20, 2012

CHEKA TARATIBU...

Jamaa mmoja amekufa ghafla na kupelekwa motoni. Shetani akakutana naye na kumuonesha milango mitatu na kumwambia lazima achague chumba kimoja cha kuishi kipindi chote humo.
Shetani akafungua mlango wa kwanza. Ndani ya chumba hicho kulikuwa na watu waliosimama huku wakikaribia kuzama kwenye kinyesi cha ng'ombe kilichofika shingoni. Jamaa akasema: "Hapana, tafadhali nioneshe chumba kingine."
Shetani akamuonesha chumba kingine na humo akaona watu wamesimama huku kinyesi cha ng'ombe ikiwafikia puani. Jamaa akasema tena: "Hapana."
Mwisho shetani akamuonesha chumba cha tatu na cha mwisho. Safari hii kulikuwa na watu wamesimama kinyesi cha ng'ombe ikiwafikia kwenye magoti huku wakinywa chai na maandazi. Hapo jamaa akasema, "Nachagua chumba hiki." Shetani akamjibu, "Sawa." Jamaa akaingia na kupewa kikombe cha chai na maandazi. Shetani akageuza kichwa chake na kusema, "Haya, mapumziko ya chai yamekwisha. Zamisheni tena vichwa vyenu kwenye kinyesi cha ng'ombe kama siku zote!" Duh...

No comments: