Sunday, April 15, 2012

CHEKA TARATIBU...

Kibaka mmoja baada ya kukurupushwa usiku wa manane na wananchi wenye hasira akijaribu kuiba kaamua kujificha kwenye pipa la takataka maeneo ya Tabata Liwiti. Huku wakiwa na usongo kundi la wananchi likafika mpaka kwenye lile pipa na kuanza kujiuliza alikopotelea yule kibaka. Mmoja akasema, "Haiwezekani atupotee hivihivi." Mwingine akadakia, "Mshenzi sana yule, leo angetutambua." Mzee mmoja naye akaongezea, "Pengine lilikuwa jini lile, mbona limeyeyuka ghafla." Kijana wa kwanaza akamalizia kwa hasira, "Tena usikute ni shoga yule." Mara wakashitukia mfuniko wa lile pipa ukifunguka na kutokeza yule kibaka, "Oyaaa, matusi yote nimevumilia lakini hilo la shoga sikubali. Shoga mwenyewe bwana." Pata picha ilikuwaje...

No comments: