CHEKA TARATIBU...

Jamaa kaingia msikitini ghafla wakati wa sala  na kuuliza kwa sauti, “Nani Muislamu safi hapa?” Wote kimyaa. Baada ya kurudia zaidi ya mara tatu bila majibu akaamua kumchukua kijana aliyekuwa jirani yake na kutokomea naye. Baada ya dakika kadhaa jamaa akarudi tena pale msikitini. Akauliza tena huku sasa mkononi akiwa na kisu chenye damu, “Nani Muislamu safi hapa?” Kama mwanzo hakupata majibu licha ya kuuliza zaidi ya mara tatu. Ndipo jamaa akasema, “Yule mwenzenu niliyemchukua anajua kuchinja tu, hajui kuchuna ngozi mbuzi!” Aah, hapo waumini wakamfuata na kila mtu akawa tayari kumpa msaada alioutaka. Kweli jambo usilolijua…

No comments: