MAMA NA BINTI YAKE WABAKWA, MTOTO AUAWA KIKATILI...

Mama Moulkheir Mint Yarba akiwa ameketi kwenye sofa na bintiye, Selek'ha. Pichani chini ni eneo lililo kwenye jangwa nchini Mauritania ambako biashara ya utumwa ilikuwa ikiendeshwa.
Inasikitisha wanaposimulia jinsi walivyotendewa visivyo, huku wakiwa wamekaa kwenye sofa tena ndani ya chumba kisichoeleweka katikati ya jangwa lililotelekezwa huko Mauritania.
Na kwa mpangilio usioeleweka vizuri lakini haikuwa mbali na simulizi ya kutisha ambayo Moulkheir Mint Yarba na binti yake Selek’ha wanayoweza kusimulia.
Simulizi yao ya kushambuliwa, kubakwa, utumwa na mauaji ya watoto wao ni moja ya mambo ambayo huwezi kuamini kuwa yametokea kwenye karne hii ya 21.
Lakini moja sehemu za simulizi zao waliyowaeleza wachunguzi wa CNN kuhusu utumwa ni kwamba sio ngeni sana masikioni.
Mnamo mwaka 1981, Mauritania ilikuwa nchi ya mwisho duniani kukomesha biashara ya utumwa. Kumiliki binadamu haikuwa jinai hadi mwaka 2007 sheria ya kuzuia biashara ya utumwa ilipofanikiwa kufanya kazi.
Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa asilimia 10 hadi 20 ya idadi ya watu milioni 3.4 wanaishi utumwani.
Moulkheir, ambaye ana zaidi ya miaka 40, alizaliwa utumwani na kutumia maisha yake yote ya utotoni kumhudumia mmiliki wake.
Alipofikia umri wa mwanzoni kuitwa mwanamke, mmiliki wake alimpeleka mashambani na kumbaka kwa mara ya kwanza.
Miaka michache baadaye, akakabidhi wake  watoto watano kwa mmiliki huyo, wote wakiwa wamezaliwa katika utumwa.
Kutokana na utamaduni wa Mauritania ulivyo, Moulkheir hakupata fursa ya kuhoji kwanini anafanyiwa hivyo.
“Nilikuwa kama mnyama ninayeishi na wanyama,” alimwambia John D. Sutter wa CNN wakati alipotembelea nchi hiyo Desemba mwaka jana ikiwa ni sehemu ya mtandao huo katika Mradi wa Uhuru, wenye lengo la kupambana na utumwa wa kisasa.
Tukio lisilo la kawaida ambalo hatokaa akalisahau maishani ni siku ile ambayo majira ya mchana akirejea nyumbani kutoka kuchunga mbuzi.
Ndipo alipokuta binti yake amelala kwenye vumbi nje ya kibanda chake akiwa tayari amekufa, binti mdogo ambaye ndio kwanza alikuwa anaanza kutambaa.
Mmiliki wa Moulkheir na baba wa binti huyo walimtupa mtoto huyo akafie nje.
Anasimulia, mmiliki akamweleza kuwa atafanya kazi haraka zaidi bila kuwa na mtoto huyo mgongoni.
Moulkheir akaamriwa amzike mwanae baada ya baba wa motto kugoma.
“Aliniambia kwamba roho ya mtoto yule ilikuwa ni ya mbwa,” amesema.
Alichoweza kufanya mwisho wa siku ni kumzika mwanae kwenye kikaburi chembamba bila maombolezo yoyote.
“Ni machozi yangu tu ndiyo yaliyonifariji,” aliwaeleza wanaharakati wanaopinga utumwa ambao baadaye walimsaidia kumtoa utumwani na kuwa huru.
“Nilimlilia sana binti yangu na mazingira niliyokuwamo. Badala ya kuelewa uchungu niliokuwa nao, wakaniamuru ninyamaze.”
Moulkheir alijaribu kuendelea na maisha yake. Baada ya kumiliki mtu mwingine ambaye aliuawa mwaka 2007, kikundi cha wanaharakati wakaingilia kati na hivyo naye akajikuta yuko huru.
Lakini furaha yake ilidumu kwa muda mfupi. Yeye na wanawe wakachukuliwa kufanya kazi kwa Kanali wa zamani wa jeshi la Mauritania. Hakukuwa na kazi. Badala yake familia ikaangukia tena utumwani. “Alibadilika na kuwa mtu mbaye sana,” anasema Moulkheir. “Alinipiga na kulala na binti zangu. Angeweza kuwapiga risasi vichwani.”
“Selek’ha alikuwa akipokea kipigo tangu akiwa na miaka 13 na muda mfupi baadaye akaanza kubakwa. Alikuja kupata ujauzito akiwa na miaka kati ya 15 na 16.
Binti huyo akaamini kwa kuwa sasa ni mjamzito basi mmiliki huyo atabadilika na kumhofia yeye na mwanae tumboni.
Haikuwa hivyo. Mimba ilipofikisha miezi tisa akampakia kwenye pick-up na kuendesha ovyo gari hiyo kwa mwendo mkali kwenye njia chafu yenye mashimo.
“Walinichukua kwenye gari na kuniendesha kwa vurugu,” alisema binti huyo. “Na motto akatoka tumboni akiwa amekufa tukiwa bado njiani.”
Kwa msaada wa shirika la wakimbizi la SOS, kikundi cha wanaharakati kilichoanzishwa na mmiliki wake wa mwanzo na mtumwa mmoja, hatimaye wote wakafanikiwa kutoroka.
Moulkheir na Selek’ha sasa wanaishi kwenye chumba kimoja mjini Nouakchott, Mouritania na kuhudhuria masomo katika shule moja ya jirani iliyoanzishwa na SOS.
Lakini wote wamebaki hawaelewi kuhusu haki yao na wanakusudia kuwafikisha mahakamani wamiliki wao wawili.
“Ninataka haki – haki kwa ajili ya binti yangu aliyeuawa, na haki kwa muda wote walionipiga na kunidhalilisha,” Moulkheir aliiambia CNN.
“Nataka haki kwa kazi zote nilizowafanyia. Nataka wote wawajibishwe. Simwogopi yeyote.”
Shule hiyo inafundisha watumwa wote walioachiwa huru mbinu za kuwasaidia waweze kuishi na kuendeleza maisha yao.
Selek’ha, sasa na miaka 18, amesema masomo hayo yamebadili maisha yake.
“Nataka kujua jinsi ya kushona, kisha nataka nipate mashine yangu ya kushonea,” ameeleza. “Baadaye, nataka kufungua duka.”
SOS lilianzishwa na Boubacar Messaoud, ambaye naye aliachiwa huru kutoka utumwani, na Abdel Nasser Ould Ethmane, aliyekuwa mmiliki watumwa.

No comments: