Padri mmoja anasafiri usiku kwa gari lake aina ya Corolla Limited kutoka Makambako kuja Dar es Salaam kwa shughuli za kikanisa.
Akiwa njiani mara akasimamishwa na askari wa usalama barabarani kwenye kizuizi kilichopo eneo la Ndiuka, kilomita chache kutoka Iringa Mjini.
Baada ya kusimama, yule askari akaanza kuulizia kitu kimoja kimoja ilimradi tu apate kosa ili amtoe kitu kidogo. Kuona kila anachouliza Padri anacho, kama kawaida yao bwana ‘wazee wa feva’ huwa hawakosi sababu ndipo akauliza, “Sasa kwanini unaendesha gari peke yako usiku, hujui ni hatari? Nakuandikia ulipe faini kwa kosa hilo.”
Kwa kujiamini kabisa Padri akajibu, “Hapana, siko peke yangu. Humu nasafiri na Yesu, Maria, Yosefu, malaika na mitume wote kumi na mbili. Hivyo afande usihofu niko salama kabisa.”
Hapo Yule askari akaruka juu na kusema kwa ukali, “Enheeee, nakuandikia kosa hilo sasa. Ume-ovalodi yaani umepakia abiria wengi kuliko uwezo wa gari!”
No comments:
Post a Comment