BINTI WA WHITNEY APATA ULAJI...

Tyler Perry (kushoto) na Bobbi Kristina Brown.
Tangu kifo cha mama yake Whitney Houston amekuwa akijihisi ‘amepoteza’, lakini Bobbi Kristina hatimaye ana kila sababu ya kutabasamu tena.
Binti huyo mwenye miaka 19 amefanikiwa kupata nafasi kushiriki kwenye tamthiliya ya  “For Better Or Worse” inayoongozwa na Tyler Perry kwenye kituo cha televisheni cha TBS.
Kwa mujibu wa mtandao wa RadarOnline.com, Bobbi alipata nafasi hiyo kupitia kwa rafiki wa Perry, ambaye aliongea kwenye msiba wa  mama yake miezi miwili iliyopita.
Perry amempa nafasi ya kushiriki katika shoo yake kwenye runinga, ambapo imeelezwa amechaguliwa kwa ajili ya msimu wa pili wa tamthiliya.
Imeelezwa kuwa kwenye msimu wa pili wa tamthiliya hiyo, Bobbi atacheza kama binti wa anayekwenda na wakati anayefanya kazi kwenye saluni moja inayoendeshwa na Angela Williams, ambaye amecheza kama Tasha Smith.
Tamthiliya hiyo ya vichekesho, asili yake ni kutoka kwenye filamu za Perry zilizotamba sana za ‘Why Did I Get Merried?’ na ‘Why Did I Get Married Too?’
Hii itakuwa nafasi yake ya kwanza Bobbi kubeba majukumu kama muigizaji.
Bahati hiyo imekuja wakati muafaka, ambapo ripoti za karibuni zimesema kuwa amekuwa akijiona kama hana msaada tangu kifo cha mama yake na kupoteza nafasi za kufanyia kazi ndoto zake za kuja kuwa mwimbaji na kuigiza.
Vyanzo vya habari vinasema: “Kila mmoja anamwogopa Bobbi.
“Bobbi hataki msaada wa yeyote. Amepotea.”
Bobbi amewahi kupelekwa hospitali kutokana na matatizo yanayohusiana na  msongo wa mawazo siku chache baada ya mwimbaji wa wimbo wa ‘I Will Always Love You’ kufariki ghafla.
Baba yake Bobby Brown ambaye hivi karibuni alikamatwa kwa kuendesha gari huku akiwa amelewa, hajachangia chochote kwenye mambo haya ya Bobbi.

No comments: