BREAKING NEWS!!
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeendelea kukitesa Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya usiku wa kuamkia leo mgombea wake, Joshua Nasari kushinda kiti cha Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki.
Nasari amefanikiwa kumbwaga kwa mbali mpinzani wake kutoka CCM, Sioi Sumari kwa kura 32,972 dhidi ya kura 26,757 alizopata mpinzani wake.
Habari nyingine zinasema CHADEMA imefanikiwa kuibwaga tena CCM katika uchaguzi wa kiti cha udiwani Kirumba.
No comments:
Post a Comment