1: Nathaniel Grant. 2: Kazeem Kolawole. 3: Anthony McCalla. 4: Duka ambamo Thusha alipigwa risasi. 5: Watuhumiwa wakikatiza mtaa na baiskeli zao muda mfupi kabla ya kuanza kurusha risasi. 6: Thusha akiwa ameanguka chini dukani baada ya kupigwa risasi kifuani. 7: Thusha akiwa mwenye furaha kabla ya shambulio lililozima ndoto zake. 8: Thusha akiwa na mama yake pamoja na ndugu zake.
Sekunde kadhaa wakati akiwa anacheza dukani kwa mjomba wake, binti wa miaka mitano alishitukia risasi ikitua kifuani mwake katika mapambano ya kutupiana risasi kati ya makundi mawili ya wahuni.
Thusha Kamaleswaran alijikuta yuko katikati ya majibizano ya risasi katika jaribio la kuuana pale risasi ilipotua kifuani mwake akicheza dukani mjini Stockwell, kusini mwa London.
Mara mbili moyo wake ulisimama kufanya kazi pale madaktari wasio na mipaka walipokuwa wakimuwahisha hospitali katika kujaribu kuokoa maisha yake. Thusha sasa atabaki kuwa mlemavu kwa maisha yake yote baada ya kupooza.
Mpaka sasa wafuasi watatu wa kundi maarufu za uhalifu wanashikiliwa na polisi wakikabiliwa na kifungo cha miaka kadhaa jela kutokana na shambulio hilo.
Nathaniel Grant, mwenye miaka 21, Kazeem Kolawole, miaka 19, na Anthony McCalla, miaka 20, wanahusika kwenye mapambano hayo ya kutupiana risasi yaliyolipuka na kunaswa kwenye kamera za CCTV wakati yakianza.
Wavamizi waliokuwa wakiendesha baiskeli waliwakimbiza wafuasi wa genge pinzani hadi dukani humo na kuzingira duka kabla ya Grant kufyatua risasi mbili mlangoni kwa kutumia bastola yake.
Roshan Selvakumar mwenye miaka 35 anayeishi ghorofani kwenye jengo hilo, ambaye alikuwa akinunua bidhaa alipigwa risasi ya uso lakini katika namna ya ajabu alinusurika kifo japo inaelezwa kuwa kuna mabaki ya risasi yaliyobaki kwenye fuvu lake.
Wavamizi hao walikuwa wafuasi wa genge la Guns And Shanks (GAS) lenye makazi yake Brixton ambao walikuwa wakiwasaka vijana wa genge la All Bout Money (ABM) lenye makazi yake kwenye mji jirani wa Stockwell.
Grant na Kolawole inadaiwa walitambuliwa kimakosa na McCall aanadhaniwa pia kuwa alihusika kwenye tukio moja la uporaji hivi karibuni.
Lakini Mahakama ya Old Bailey imewatia hatiani kwa makosa ya kujeruhi watu wawili kwa kudhamiria na jaribio la kutaka kumuua mfuasi wa kundi hasimu, Roshaun Bryan.
Watuhumiwa wengine hawajatambulika. Watuhumiwa walisimama huku mikono yao ikiwa mifukoni wakati wakitajwa majina yao bila kuonyesha hisia zozote.
Mama wa Thusha, Sharmila, na baba yake, Jeyakumar Ghanasekaram, walikaa kimya wakifuatilia wakati watuhumiwa hao wakisomewa mashitaka mahakamani hapo.
Akielezea madhara yaliyotokana na tukio hilo katika taarifa iliyosomwa mahakamani hapo, Sharmila anaeleza kuwa alikuwa akitokwa machozi kila alipomfikiria binti yake na hatima yake.
"Ni ngumu kwa kila mmoja nyumbani kuona binti asiye na hatia aliyekuwa mtundu kama panya, sasa amepooza," anasema Mwendesha Mashitaka Michelle Nelson, akisoma taarifa kutoka kwa Bibi Kamaleswaram kwa niaba ya familia.
"Alikuwa binti mpenda michezo, mwenye furaha wakati wote na mwenye bashasha na alikuwa mwanafunzi mzuri shuleni."
Grant aliinamisha kichwa chini wakati mtuhumiwa mwenzake hakuonesha hisia zozote taarifa hiyo ilipokuwa ikisomwa mahakamani.
Bi Nelson aliongeza: "Alichosema ni kwamba madhara ya tukio hilo hayapimiki kwa familia hiyo.
"Hawezi kuanza kuelezea mshituko alioupata wakati wa majibizano hayo ya risasi, na kwamba watoto wake wote alikuwapo dukani wakicheza na mara Thusha akaanguka na kugaagaa chini huku akilia na kulalamika kuwa anashindwa kuinua miguu yake."
Anaelezea kwamba aliambiwa na madaktari wasio na mipaka kuwa Thusha ana maradhi ya moyo na kwa wakati huo hawakuweza kujua kama atapona.
"Alielezwa kuwa Thusha 'alikufa' mara mbili akiwa njia kupelekwa hospitali baada ya mapigo yake ya moyo kusimama. Kwa siku kadhaa baada ya tukio, familia ilihamia hospitali huku wakishindwa kabisa kupata usingizi wala kula chakula."
"Mama yake anasema anashindwa kabisa kufikiri. Kumwona mwanae amelala kwenye kitanda hospitalini wanakata kabisa tamaa. Anasema anashindwa kufikiri wakati huu mbaya zaidi kutokea katika maisha yake akifafanua jinsi familia inavyopata wakati mgumu kuunganisha mambo."
Bi. Kamaleswaran anasema ndoto za binti yake kuwa mwimbaji zimezimika ghafla.
Genge hilo lilikuwa likijaribu bunduki zao jirani na nyumba yo mjini Brixton kabla ya kuingia kwenye mapambano ya kuwasaka mahasimu wao Machi 29, mwaka huu.
Grant na Kolawole walivamia mtaa wakiwa kwenye baiskeli za mashindano wakati McCalla alikuwa akiendesha baiskeli ya kike ambayo aliitelekeza baada ya mapigano hayo.
Olumayoura Adadegbuyi, karani wa duka la William Hill alisikia kelele kwenye barabara la Stockwell, kusini mwa London, wakati wapanda baiskeli waliokuwa wamejifunika sura zao na kujificha kwenye choo cha duka hilo.
Thusha alikuwa akicheza na kaka yake mwenye miaka 12 na mdogo wake wa kike mwenye miaka mitatu chumbani kwenye duka la Mvinyo na Chakula la Stockwell.
Mama aliwapeleka watoto dukani hapo kutoka nyumbani kwao Hainault, mashariki mwa London kumpitia mume wake aliyefahamika kwa jina la Sassi, ambaye alikuwa akifanya kazi mpaka majira ya usiku.
Ilikuwa majira ya saa 3 usiku wakati Thusha na wenzake waliposhuka dukani kuangalia kelele na milio ya risasi, huku Bi Kamaleswaran akiwafuata kwa nyuma.
Punde akashuhudia tukio la kutisha pale alipomwona binti yake mdogo akianguka sakafuni.
"Kufuatia kelele hizo kuendelea, katika kujaribu kumkinga mwanangu, nami nikakimbilia dukani," anasema.
"Pale nikamwona Thusha akikaribia kuanguka sakafuni akionekana kama miguu yake imepoteza mawasiliano. Nilimudu kumdaka na kuzuia asianguke. Kisha Thusha akaniomba nimsaidie kunyanyuka.
"Nilijaribu lakini sikuweza."
Kwenye kipande cha video kilichodumu kwa dakika moja, Bryan anaonekena akiingia dukani kwa kazi akiwa na Christopher Munsaka. Wakajipanga na kuanza kurusha chupa mlangoni.
Selvakumar anaonekana akijaribu kufunga mlango ambapo badala yake akaanguka huku akichuruzika damu.
Thusha anaonekana akicheza kwenye duka hilo linalomilikiwa na mjomba wake, akiwa amevalia nguo nyekundu kabla ya kuelekea mlangoni.
Walengwa wa mapambano yao wakitoweka eneo la tukio wakati akipelekwa ndani ya duka kwa usalama zaidi.
Akielezea vurugu ndani ya duka mjomba wa Thusha
Mahadavan Vikneswaran aliongeza: "Niliweza kumsikia Sassi akipiga kelele, 'Hapana, hapana, hapana' huku akirudirudia.
"Nilisikia kelele nyingine pia. Nikamsukuma kando dada yangu na kukimbilia chumba cha kuhifadhia bidhaa.
"Nikaona vijana wawili weusi kwa jokofu ambako vilevi vinahifadhiwa na kuanza kurusha chupa kuelekea mlangoni.
"Niliwasikia wakipiga kelele lakini sikuweza kuona waliyekuwa wakimpigia kelele.
Wakati Ghanasekaram akipiga simu polisi, Vikneswaran alimwona Thusha akikimbilia dukani na kusimama karibu naye.
Pengine alitaka kuona nini kinaendelea,' alisema.
"Nikagundua Thusha analia na kumuona akianguka sakafuni kando yangu. Haraka nikamnyanyua na kumkimbizia chumba cha nyuma ya duka hilo.
Wakati huohuo, polisi wameandaa mpango kabambe wa kuanzisha harambee kuchangia gharama za matibabu ya Thusha.
Binti huyo amekuwa akitumia muda wake mwingi hospitalini mwaka mmoja baada ya tukio ka kupigwa risasi ambalo limebadili kabisa maisha yake.
Anaruhusiwa kwenda nyumbani mwishoni mwa wiki tu na wazazi wake wamekuwa wakijipanga kumuhamishia nyumbani kwa kuweka vifaa vyote muhimu.
Binti huyo ambaye sasa ana miaka sita, anatarajiwa kutumia kiti cha magurudumu muda wote baada ya risasi kuathiri uti wake wa mgongo.
Askari Upelelezi Jim Redmond, Konstebo Richard Williamson na Konstebo John Codd, ni kati ya maofisa 20 na wafanyakazi wa jeshi la polisi ambao watashughulikia harambee hiyo.
Washirika hao wamedhamiria kuchangisha kadri wanavyoweza kugharimia vifaa vya kitaalamu kwa ajili ya matumizi ya Thusha atakapokuwa nyumbani.
Wamefungua pia akaunti maalumu kwa jina la Thusha ambapo walioguswa watapitisha fedha zao huko kwa ajili ya kugharimia matibabu ya binti huyo.

1 comment:
[url=http://www.pascherdoudounesenligne.fr]canada goose doudoune[/url] Baby Lulu is a brand of designer-inspired clothing made specifically for children and toddlers below the age of five. [url=http://www.pandoraonilnestore.co.uk]pandora uk[/url]
[url=http://www.canadagoosedame.eu]billig canada goose[/url] omswzhtn
[url=http://www.franceuggboots.eu]www.franceuggboots.eu[/url] [url=http://www.franceuggboots.eu]fausse ugg[/url]
Post a Comment