Thursday, March 29, 2012

CHEKA TARATIBU...

Jamaa mmoja akiwa nyumbani na mkewe wanaangalia filamu, mara wakavamia majambazi wawili na kuanza kupiga huku wakiwanyooshea bunduki.
Huku wakiendelea kuwapiga jamaa na mkewe, majambazi hayo yaliulizia wapi zilipo pesa ama sivyo wangewaua.
Kwa hofu kubwa, jamaa akanyoosha kidole kuelekea chumbani akiashiria ndiko ziliko fedha na bila kuchelewa jambazi moja likaenda na kufanikiwa kupata kiasi kikubwa cha pesa.
Baada ya kutoka jambazi moja likawaamrisha mume na mke wajitambulishe majina yao kabla hajaanza kuwafyatulia risasi.
Ndipo mke wake kwa woga akaanza kujitambulisha, "Mimi naitwa Mariam." Lile jambazi huku likiwa limeelekeza mtutu usoni mwa yule mwanamke likajibu, "Safi sana, sitakuua kwa sababu una jina kama la mama yangu mzazi." Kisha lilamgeuzia mtutu yule jamaa, "Enhe, na wewe fala?" Jamaa huku akichuruzika mkojo akajitambulisha, "Naitwa Bakari, ila kazini wananiitaga Mariam." Duh, usifanye mchezo na kifo...

No comments: