Friday, March 2, 2012
TANESCO NA LUKU YAO AIBU TUPU!!!
Walipoomba kupandisha bei ya umeme, wengi tulilalamika lakini tukapiga moyo konde kwa imani moja tu kwamba pengine huduma zingekuwa bora. Aah wapi! Hakuna lolote, jana usiku wakazi wengi wa Dar es Salaam wameshuhudia 'uswahili' uliopitiliza katika mtandao wa Tanesco wa kuuzia umeme wa LUKU ambapo walilazimika kusimama kwenye misururu mirefu kwa zaidi ya masaa manne hadi sita wakisubiri kuuziwa umeme kwenye vituo vya Mwananyamala 'A', Zizzou Fashion Oilcom Victoria, Oilcom Sayansi n.k. Pichani ni kituo cha Luku Kariakoo. TANESCO BADILIKENI JAMANIIIIIIIII....
This is a blog that brings you hot news that aims to educate the community about various things including sports, culture, art, entertainment and social. This blog does not involve political issues at all. We ask for your cooperation and to contribute opinions on the various information we bring to you.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Tanesco wameshindwa kazi. Waachie ngazi.
Post a Comment