MWIMBAJI WA THE MONKEES AFARIKI...


Ranchi ambamo Davy Jones alianza kujisikia vibaya na kukimbizwa hospitali.

Mwimbaji na kiongozi wa kundi la The Monkees, Davy Jones amefariki dunia mapema leo kwa ugonjwa wa moyo akiwa na umri wa miaka 66, imefahamika.

Maofisa wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Florida wamethibitisha kifo hicho kwa kusema walipokea simu kutoka Hospitali ya Martin Memorial ikieleza kwamba Jones amefariki dunia.

Tumeelezwa kwamba Davy alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo yaliyomzidia akiwa kwenye ranchi yake jirani na nyumbani kwake mjini Florida, ambapo alikwenda kuangalia farasi wake. Davy alianza kujisikia vibaya wakati akiwa ndani ya gari lake ndipo waangalizi wa ranchi hiyo walipomwona na kumpa msaada.

Waangalizi wa ranchi hiyo waliwaeleza wapelelezi kuwa mwimbaji huyo alianza kulalamika kwamba hajisikii vizuri na alikuwa akipumua kwa shida. Watu wa huduma ya kwanza waliitwa na kumchukua Jones hadi kwenye hospitali iliyo jirani na hapo ambapo walielezwa kwamba amekwishafariki.



Mamlaka za Florida zimesema kwamba hakuna anayeshukiwa kuhusika na kifo hicho na kwamba ni kifo cha kawaida tu.


Jones ameacha mke, Jessica na watoto wa kike wanne kutoka kwenye ndoa zake zilizotangulia. Alimuoa Jessica Pacheco  kama mke wa tatu.

Jones alijiunga na kundi la The Monkees mwaka 1965 akiwa pamoja na Micky Dolenz, Michael Nesmith na Peter Tork ... na kwa pamoja wakaibuka na vibao vikali vitatu vilivyotikisa vya "Daydream Believer," "Last Train to Clarksville" na "I'm a Believer."

No comments: