1: Hoteli ya Hilton iliyoko mjini Manchester ambayo inadaiwa Balotelli huwa nakwenda kula maisha. 2: Balotelli (kushoto) na Carlos Tevez wakitoka uwanjani mara baada ya kumalizika pambano kati ya Man City na Wigan Athletic. 3: Eneo analoishi mama mzazi wa Balotelli. 4: Baa ya The Tudor. 5: Balotelli (kushoto) akicheza kitandani pamoja na mama yake mzazi na mdogo wake Enoch. Hapa alikuwa na miaka kumi alipotembelewa na mama yake.
Mama wa mshambuliaji wa timu ya Manchester City ya England, Mario Balotelli amehamishia makazi yake kwenye eneo lenye maisha magumu kinaporushwa kipindi cha televisheni cha ‘Shameless’ akijaribu kuunda upya mahusiano na kijana wake huyo aliyemtelekeza akiwa na miaka miwili tu.
Mama huyo aliyezaliwa Ghana, Rose Barwuah, mwenye miaka 46, alihamia Wythenshawe mjini Manchester akitokea Italia na kuishi kwenye nyumba ya kupanga.
Lengo lake ni kujaribu kutafuta ukaribu, huku Balotelli anayelipwa Pauni 120,000 kwa wiki amekuwa akionekana eneo hilo akiwa ndani ya gari lake aina ya Bentley GT, na kumpeleka mama yake mzazi kwenye maduka au kupiga naye kinywaji kwenye baa za jirani.
Nyumba anayoishi mama huyo inayogharimu kiasi cha Pauni 550 kwa mwezi, iko mbali na jumba la kifahari analoishi nyota huyo ambalo humgharimu Pauni milioni 3 ama wakati mwingine amekuwa akila maisha kwenye Hoteli ya Hilton ya mjini Manchester.
Balotelli aliasiliwa akiwa na miaka miwili baada ya wazazi wake waliokuwa wakifanya kazi za kujitolea kuamua kumkabidhi kwa familia yenye uwezo kutokana na wao kukabiliwa na hali ngumu ya maisha.
Familia ilikuwa ikijitahidi kujikwamua kiuchumi ili kumudu japo kulipa pango kwenye ghorofa moja mjini Brescia, Italia, na Mario wakati huo alikuwa ndio anapata nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji wa utumbo mkubwa ulioigharimu familia hiyo fedha nyingi.
Kipindi cha nyuma nyota huyo wa Ligi Kuu ya England kuna wakati alikuwa akirejea kucheza na mdogo wake, Enoch, lakini hali ilibadilika kadri miaka ilivyokuwa ikisonga mbele.
Wakati mama yake mzazi alipohamia mjini Manchester, mwanasoka huyo aking’aka kwamba amefuata pesa zake tu na si kingine.
Lakini majirani waliliambia gazeti la The Sun: “Mario ameanza kujirudi na kumtembelea mara kwa mara. Wakati mwingine amekuwa akimnunulia mahitaji yake.
“Amekuwa mkarimu kwake na wakati mwingine amekuwa akisaini vifaa mbalimbali vya michezo. Amekuwa akifika kwenye baa ya jirani ya The Tudor, na wakati mwingine kumlipia vinywaji. Inapendeza kuona kwamba Mario na Rose wamekuwa wamoja tena.”
Aliongeza: “Rose anafanya yote haya kuonesha kuwa hayuko hapa kwa ajili ya fedha. Hii ni nyumba anayoweza kumudu kulipa pango. Anachotaka kukaa na kijana wake na kumfahamu vizuri.
“Rose ameshapazoea hapa. Anafanya kazi kwenye soko la Wythenshawe, akidamka kabla ya saa 12 alfajiri kupanga vifaa kwa ajili wafanyabiashara.”
Baba mzazi wa Balotelli, Thomas inasemekana yuko nchini Ghana, akijiandaa kuhamia Manchester siku za usoni.
Binti wa Rose, Angel, mwenye miaka 13 naye pia amehamia Uingereza pamoja na mama yake.
Jirani mwingine ameliambia The Sun kuwa Rose ni “mwanamke mcha Mungu anyekwenda kanisani kila Jumapili.
“Alichokuwa akiomba siku zote ni kuungana na kijana wake na sasa inaonekana kama sala zake zimejibiwa.”

No comments:
Post a Comment